RUFAA YA DHAMANA YA MBOWE NA MATIKO KUANZA KUSIKILIZWA FEBRUARI 18

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa rufaa ya kupinga dhamana iliyokatwa na upande wa mashtaka dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019 katika Mahakama ya Rufaa.

Taarifa hiyo umetolewa leo Alhamisi Januari 31, 2019 na wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wankyo amedai kuwa kesi lilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanasubiri uamuzi wa mahakama ya rufaa.

"Washtakiwa wote wapo mbele ya mahakama yako na kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kuna rufaa iliyopo mahakama ya rufaa ambayo bado haijasikilizwa, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa, wakati tukisubiri maamuzi ya mahakama ya rufaa,” amedai Wankyo.

Amedai kuwa rufaa hiyo ya kupinga dhamana iliyokatwa na upande wa mashtaka itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019.

Na Hadija Jumanne, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post