WAZIRI WA MAMBO YA KIGENI POMPEO ASHAMBULIA SERA ZA OBAMA

Ägypten | Mike Pompeo (picture-alliance/dpa/AP Photo/A. Nabil)Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo aliyasema  hayo katika ukosoaji  mkubwa  wa  sera  za  rais  huyo  wa  zamani  licha  ya hatua  za  mkuu  wa  Pompeo  rais Donald Trump  kuamua kuviondoa  vikosi vya  jeshi  la  Marekani  kutoka  Syria.

"Tunahitaji  kutambua  ukweli  huu kwasababu  iwapo  hatutafanya hivyo, tutafanya  makosa  ya  uchaguzi kwa  hivi  sasa  na  hapo baadaye Na uchaguzi  wetu , kile  tutakachokichagua  leo kina athari kwa  mataifa na  kwa  mamilioni  ya  watu , kwa  usalama  wetu, kwa ufanisi  wa  uchumi wetu, kwa  uhuru  wetu , na  ule  wa  watoto wetu." Alisema Pompeo
Katika  hotuba  ambayo  aliitoa  katika  chuo  kikuu  cha  Marekani mjini  Cairo, Pompeo  alijitenga  na utamaduni  wa  kidiplomasia  wa Marekani  wa  kuepuka kutangaza  hadharani  mizozo  wa  ndani nchini  Marekani  kwa  kumshambulia  Obama  katika  mahali ambapo  mtangulizi  huyo  wa  rais  Trum  alitoa  hotuba  ya kihistoria  yenye  lengo  la  kuimarisha  mahusiano  na  ulimwengu wa  Kiislamu.

 Pompeo ameiwasilisha  Marekani  kuwa  ni  nguvu  ya kufanya  mazuri  katika  mashariki  ya  kati,  na  kudokeza  kwamba Obama  aliiona  Marekani  kama " nguvu  inayoitaabisha  mashariki ya  kati".

Baadhi  ya  maafisa  wa  zamani  wa  Marekani  na  wachambuzi wamemshutumu  mwanadiplomasia  huyo  wa  ngazi  ya  juu  wa Marekani  kwa  kusoma  vibaya  historia  na  kujificha  katika mapenzi  ya  binafsi  ya  Trump  kupunguza  jukumu  lake  katika eneo  hilo.

Chanzo:Dw

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527