Tanzia : MUIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA AFARIKI DUNIA


Marehemu Mama Abdul enzi za uhai wake.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba, amesema msiba wa muigizaji Mama Abdul ni msiba ni pigo kwenye kiwanda kizima cha filamu Tanzania na wasanii wanatakiwa kuungana kuifariji familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.

Akiongea kwa njia ya simu Mwakifamba amesema amepokea taarifa za msiba huo akiwa safarini hivyo hajaongea na familia juu ya chanzo cha msiba huo lakini anafanya mawasiliano usiku huu ili kujua undani wake.

''Nipo safarini ndio nimefika usiku huu, kuhusu chanzo cha kifo chake bado sijawasiliana na familia lakini niwaombe tu wasanii wenzangu tuungane katika kipindi hiki kigumu cha kumhifadhi mwenzetu kisha mimi nafanya mawasiliano na familia na nitatoa taarifa rasmi'', amesema.

Kwa mujibu wa taarifa ya mapema iliyotolewa na Kamati ya Matukio Maadili na mikataba ya Chama cha waigizaji TDFAA (M) Kinondoni na Ubungo ilieleza kuwa msiba huo umetokea mchana leo nyumbani kwake Mburahati na msiba upo hapo nyumbani.

Aidha ilifananua kuwa taarifa juu ya taratibu za mazishi itatolewa baadaye baada ya kikao na familia, huku wasanii pia wakiombwa kushirikiana.

Baadhi ya wasanii walioonesha kusikitishwa na msiba huo ni pamoja na JB, Riyama Ally, Johari, Monalisa na wengine.
Mtangazaji, Zamaradi kupitia ukurasa wake wa Instagramu ameandika "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa SALOME NONGE maarufu kama MAMA ABDUL."

"Kwa wasiomfahamu kama uliwahi kuangalia filamu ya KIGODORO 'kantangaze' nilibahatika kufanya nae kazi enzi za uhai wake, lakini pia kwa ambao hawajabahatika kuona filamu hiyo unaweza kumuona kupitia tamthilia ya MWANTUM kwenye stesheni ya Magic Swahili DSTV," aliandika Zamaradi huku akimalizia hiv; MUNGU amuweke mahala pema peponi Mama Abdul' Inalillahi wainailaihi Rajiun'

Kwa upande wake mama yake mzazi Monalisa ambaye anajulikana kama Natasha Mamvi ameandika TANZIA;RAFIKI YANGU KIPENZI.MZAZI MWENZANGU.MWIGIZAJI MWENZANGU SALOME NONGE (MAMA ABDUL) AMEFARIKI. NI PENGO AMBALO HALITAZIBIKA KAMWE.RIP MAMA ABDUL.

Naye Monalisa ameandika," Mama Abdul Jamani, Pumzika kwa amani tutakukumbuka daima."

Joti naye ameandika R.I.P Mama Abdull.Mimi mwanao Sina cha kuongea zaidi ya kukuombea upate mwanga wa milele, Pumzika kwa amani mama."

Kuwa Mjanja..Download App mpya ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari za michezo moja kwa moja Kwenye Simu yako

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527