MAWAZIRI WAWILI NA MKUU WA MKOA WATAKIWA KURIPOTI KWA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi waandamizi wa mkoa wa Iringa akiwemo mkuu wa mkoa huo, Ally Hapi kuripoti ofisini kwake Dodoma saa 5 asubuhi Jumatatu 7, 2019.

Wengine wanaopaswa kuwapo katika kikao hicho ni, Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo pamoja na wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri za mkoa huo.

Majaliwa alitoa agizo hilo jana Ijumaa wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyoni wilayani Mbinga mkoani Ruvuma akisema inashangaza kuona Serikali inafanya jitihada za kusambaza umeme halafu watendaji wa Serikali wanaweka vikwazo.

“Nataka waje waniambie kwa nini wanazuia nguzo, wananchi wanasubiri wao wamezuia nguzo wanasubiri posho wanaidai Serikali na wao Serikali sasa tutakutana ofisini.”

“Yaani sisi tunaahidi umeme uwake kila nyumba ya Mtanzania mpaka yule mnyonge halafu kuna mtu anazuia nguzo na miti hii tumeipanda wenyewe,” amesema.

Na Elizabeth Edward, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527