MANARA : NITAONGOZA JESHI LA POLISI KUSAKA WANAOUZA JEZI FEKI ZA SIMBA


'Kwenye mambo muhimu yanayohusu klabu yangu nipo tayari nisiangalie mpira 'Yes' nitaongoza jeshi la polisi kusaka wanaouza jezi feki''.

Ni kauli ya msemaji wa Simba Haji Manara leo alipokuwa akiongea na wana habari kuelekea mchezo wa Klabu Bingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya JS Souara Jumamosi ya wiki hii.

Katika mchezo huo, Manara amesema moja ya jambo ambalo watalitilia mkazo siku hiyo ni kuuza jezi halisi za Simba na sio feki.

''Siku ya mchezo wetu dhidi ya JS Souara nitaongoza jopo la wanasimba wenzangu kwa kushirikiana na Polisi kukamata wale wote wanaoihujumu klabu kwa kuuza jezi feki'' ameongeza Manara.

Aidha Manara amebainisha kuwa wapinzani wao klabu ya JS Souara watafika hapa nchini Januari 10, na Ijumaa watafanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa ambao ndio utatumika kwenye mchezo wa Jumamosi.

Kwa upande wa kikosi cha kwanza cha Simba kinatarajiwa kurejea Dar es salaam kutoka Zanzibar kesho asubuhi tayari kwa maandalizi ya mchezo huo.

Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post