MANARA ATOA SABABU ZA KUTOJIBU SALAMU ZA WANAJANGWANI

Simba imereja nyumbani ikiwa na kumbukumbu mbaya kichwani, ikipoteza mchezo huo kwa mabao 5-0.
Afisa Habari wa Simba, Haji Manara ambaye amekuwa akiandamwa na mashabiki wa Yanga kutokana na tambo zake, amejitokeza na kueleza sababu ambayo imepelekea ukimya wake baada ya mchezo huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa sababu iliyomfanya kushindwa kujibu ujumbe wa watani wake ni tatizo la mtandao nchini DR Congo.

"Alhamdulillah tumerejea salama nyumbani na leo tunaanza mazoezi kwa ajili ya tournament ya @SportPesaCup!!
Nitumie pia fursa hii kuwashukuru nyote mlionitakia kheri na baraka ktk siku yangu ya kuzaliwa (kumbukizi) juzi Ijumaa, ila niwaombe radhi kwa kutokujibu salaam zenu,na sababu kubwa Congo nzima haina internet kwa sasa ila maeneo machache tena kwa wakati mfupi sana!!
Niseme tu Asanteni Sana na nimefarijika mno,na hasa zile salaam zilizotoka kwa Watani zangu 
Mungu atubariki sote Insha'Allah" ameandika Manara


Kufuatia matokeo hayo, sasa Simba inakamata nafasi ya tatu katika kundi lake la D, ikiwa na alama 3 na magoli 3. Kundi hilo linaongozwa na Al Ahly iliyo na alama 4, AS Vita iliyo nafasi ya pili kwa alama 3 na JS Saoura inayoburuza mkia kwa alama moja pekee.

Baada ya kurejea nchini, Simba itaingia moja kwa moja kambini tayari kwa maandalizi ya mashindano ya Sport Pesa Seper Cup yanayotarajia kuanza kesho katika uwanja wa taifa, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu hiyo.

Simba inatarajia kukutana na AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa awali na imesema kuwa itayatumia mashindano hayo kwaajili ya kujiandaa na michuano inayoendelea ya Klabu Bingwa Afrika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527