MANARA AKERWA NA BABA YAKE AMTUMIA UJUMBE MZITO


Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amefunguka kuwa kitendo cha Baba yake mzazi, Sunday Manara ambaye aliichezea klabu ya Yanga zamani kuonekana bado akishirikiana na timu hiyo kinamuumiza.


Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo amesema kuwa hakupenda baba yake achezee klabu hiyo ya mahasimu wake wa jadi lakini hawezi kurithi ushabiki wa timu hiyo.

"Daaah, huyu ni baba yangu mzazi na nampenda sana ila hata sijui kwanini, alicheza hili timu na nnajua hivi sasa Yanga wanajitahidi kumtumia ili kunififisha mimi , lakini hawataweza, yeye ni Gongowazi mimi ni Simba. Duniani watu hurithi mali, hawarithi ushabiki wa timu", ameandika Manara.

Manara ameendelea kusema kuwa, "Baba yangu muda ni huu, achana na hiyo mitimu ya ajabu ajabu, hiyo timu unayoshabikia ni ya watu wa zamani enzi za kina Unju bin Unuki, njoo Simba kuna Chama na kina Kagere, halafu yupo MO na mwanao, baba, baba tafadhali mimi mwanao nisikilize".

Hivi karibuni Baba mzazi wa msemaji huyo, mzee Sunday Manara alizungumza na wanahabari na kutoa shukurani kwa kocha wao Mwinyi Zahera ambaye ameonesha kuibeba klabu hiyo katika kipindi ambacho timu inakabiriwa na ukata wa fedha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post