LIVERPOOL YAKUBALI YAISHE,YAGONGWA 2 - 1 NA MAN CITY


Liverpool imekubali kupoteza mchezo uliopigwa usiku huu dhidi ya Manchester City kwa kufungwa bao 2-1.


Mabao ya City yamewekwa kimiani na Sergio Kun Arguero na Leroy Sane huku Liverpool ikifuta machozi kupitia kwa Roberto Firmino.

Ushindi huo wa Man City unakuwa wa kwanza baada ya mechi tano mfululizo katika EPL kushindwa kupata matokeo mbele ya Liverpool.

Kupoteza kwa Liverpool kumeifanya ikubali kufungwa mabao mawili msimu huu EPL ndani ya mechi moja na ikipoteza mchezo wa kwanza.

Msimamo unaonesha hivi sasa Liverpool bado ipo kileleni ikiwa na pointi 54 kwa tofauti ya alama 4 na Man City iliyo na 50.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post