MBUNGE WA CHADEMA GODLESS LEMA KUJIUZULU

Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa endapo Spika wa Bunge Job Ndugai atalithibitishia bunge kuhusu kauli yake dhidi ya matibabu ya Lissu, yeye atakuwa tayari kujiuzulu.

Lema ametoa kauli hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter ambapo amejibu kauli iliyotolewa na Spika akiwa bungeni leo ambapo amesema kuwa mpaka sasa bunge limegharamia shilingi milioni 250 katika matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

"Bunge halijawahi kumlipia Mh Lissu pesa kwa ajili ya matibabu, alichokisema Mh Spika Ndugai ni upotoshaji kwa jamii na Mungu. Chama kitatoa tamko juu ya hili. Spika akiweza kuthibitisha hili, mimi nitajiuzulu Ubunge, mshahara wa Mbunge sio hisani ya Spika", ameandika Lema.
Akizungumza bungeni leo, Januari 31 Spika Job Ndugai amesema hadi sasa Bunge limeshamlipa Tundu Lissu shilingi milioni 250 kwa ajili ya matibabu yake.

Amesema hadi mwishoni mwa Desemba 2018, Lissu alikuwa amelipwa Sh207.8milioni pamoja na Sh43 milioni zilizotolewa kama mchango wa matibabu ya mbunge huyo.

Amesema kwa ujumla hadi sasa Lissu amelipwa Sh250milioni kutoka bungeni.

“Siku za mwanzo sikutaka kujibu maana niliamini kumjibu mtu aliyelala kitandani siyo vizuri kwani kuna vitu huenda vingekuwa vimempita, lakini sasa naamini ni mzima hadi anafanya ziara nje. Nalisema hili akijibu nakuja na mkeka hapa,” amesema Ndugai. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527