WAZIRI AGOMA KUTUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema hayupo tayari kutimuliwa na Rais John Magufuli kwa kushindwa kupeleka huduma za maji kwa wananchi.

Kauli ya Aweso imetokana na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya maji katika wilayani Kisarawe mkoani Pwani licha ya bajeti iliyopo.

Akizungumza leo Jumanne Januari 22, 2019 wakati wa ziara ya kikazi katika wilaya hiyo, Aweso amesema Rais Magufuli alipomteua alimpa jukumu la kuhakikisha maji safi na salama yanawafikia wananchi wote.

Kauli hiyo ya Aweso imetokana na kusuasua kwa miradi ya maji wilayani humo huku mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo akisema imeshindwa kuendelea kwa kukosa huduma ya maji.

"Tulipoteuliwa katika nafasi hizi Rais alisema anatupa wizara hii ili wananchi wapate maji na wasipopata basi atatumbua na mimi sipo tayari kutumbuliwa," amesema Aweso.


Na Cledo Michael, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527