BABA AWABAKA WATOTO WAKE WAWILI MOROGOROWatoto wawili katika kijiji cha Mangaye mkoani Morogoro, mmoja mwenye miaka nane na mwingine mwenye miaka tisa wamebakwa na mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Paulo Ilonga mwenye umri wa miaka 68 ambaye ni baba yao wa kambo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo lilihudhuriwa na mama mzazi wa watoto hao aitwaye Lucia Hando ambapo baba yao aliwachukua watoto hao usiku wakati wamelala na kuwapeleka nyuma ya nyumba na kuwafanyia kitendo hicho huku akiwatishia kuwa angewachapa.

Katika tukio lingine, wananchi wa eneo la Mikumi Kwalaza, kata ya Mikumi mkoani Morogoro wamemkamata Askari wa Jeshi la Wananchi aliyejulikana kwa jina la Godlisten Remistone mwenye umri wa miaka 46 kwa kosa la kumbaka mwanafunzi.

Askari huyo wa kambi ya jeshi ya Suku wilayani Mikumi, alikamatwa na wananchi hao baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mikumi.

"Baada ya kumkamata, alipelekwa kituo cha polisi cha Mikumi na anaendelea kushikiliwa mpaka sasa, uchunguzi unaendelea kufanyika kwaajili ya hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake", amesema Mutafungwa.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post