KCMC YASITISHA KUTOA HUDUMA YA BIMA KWA MAKAMPUNI HAYA


Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro imesitisha kutoa huduma kwa wafanyakazi wa makampuni saba yanayotumia bima za afya kutokana makapuni hayo kudaiwa zaidi ya shilingi bilioni 2.2.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mahusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo, hospitali hiyo imelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya makampuni hayo kushindwa kulipa madeni yake yanayokadiliwa kufikia Sh. Bilioni 2.2.

Chisseo ameyataja Makampuni hayo kuwa ni NSSF, AAR, Jubilee, Strategies, Ngorongoro, TPC na TANESCO ambapo amesema baadhi yake yanadaiwa fedha za tangu mwaka 2016.

“Tuna mkataba na hizi taasisi, ule mkataba unaonyesha baada ya mwezi mmoja wawe wametulipa baada ya kutoa huduma kwa wanufaika wao, hadi sasa tuna madai ya tangu mwaka 2016 mpaka sasa.

“Kwa hiyo kwetu sisi tunapata mzigo mkubwa na wakumbuke
tumekuwa tuna jukumu la kutibu watanzania ambao hawana uwezo kupitia hiki hiki kiasi kidogo ambacho wananchi wamekuwa wanachangia,” alisema Chiseo.

Alisema uongozi wa hospitali umeshatoa taarifa kwa njia mbalimbali, hivyo ni wajibu wa wanufaika hao kwenda moja kwa moja katika taasisi na mashirika hayo kuwaeleza namna ambavyo wataweza kuhudumiwa baada ya huduma kusitishwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527