UONGOZI WA YANGA WATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMUSOKO KUONDOKA YANGA

Uongozi wa klabu ya Yanga umeutolea ufafanuzi ujumbe wa kiungo wake Mzimbambwe, Thaban Kamusoko baada ya kuleta sintofahamu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kamusoko hivi karibuni aliandika ujumbe huo ukieleza kuwashukuru wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa upendo waliomuoneshea tangu ajiunge na timu hiyo.

Kamusoko aliandika ujumbe huo ambapo mashabiki wengi waliokomenti walielewa kuwa ameshaagana na mabosi wake na ikachukuliwa kuwa anaondoka Yanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari, Dismas Ten, ameibuka na kuutolea ufafanuzi kuwa Kamusoko aliandika na hakuwa na maana ya kuondoka.

Ten ameeleza kuwa ifikie wakati mashabiki wasiwe wanakariri mambo pale mtu anapoandika ujumbe wa aina kama ile, kwani si kweli kuwa anaondoka.

"Si kweli, alichokiandika hakina maana ambayo wengi wametafsiri, bado ana mkataba na Yanga na ataendelea kuwepo" alisema Ten.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527