SERIKALI YAZIMA JARIBIO LA KUMPINDUA RAIS BONGO

Waziri wa mawasiliano nchini Gabon anasema wanajeshi waaminifu kwa serikali ya Rais Ali Bongo wamefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya serikali nchini humo.


Bw Guy-Bertrand Mapangou ameambia BBC kwamba wanajeshi wanne waliohusika katika jaribio hilo wamekamatwa na mwingine wa tano anasakwa.

"Hali ni tulivu. Polisi ambao huwa hapo wamerejea na kuchukua udhibiti wa eneo lote la makao makuu ya mashirika ya redio na runinga, kwa hivyo kila kitu kimerejea kawaida," amesema.

"Walikuwa watano. Wanne wamekamatwa na mmoja yupo mafichoni na atakamatwa saa chache zijazo."

Kundi la wanajeshi nchini Gabon lilikuwa limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi na kutangaza amri ya kutotoka nje.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527