AZAM FC WAIADHIBU YANGA BILA HURUMA...CHIRWA BALAA!!Dakika 90 za mchezo wa kombe la Mapinduzi kati ya Yanga na Azam FC katika Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar zimemalizika kwa Azam FC kuiadhibu Yanga mabao 3 - 0.

Obrey Chirwa alifunga mabao mawili dakika ya 33 akipokea pasi kutoka kwa Tafadzwa Kutinyu na dakika ya 60 kipindi cha pili alifunga bao la tatu.

Ennock Atta alifunga bao la pili dakika ya 44 kwa mpira wa faulo akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kushoto uliozama moja kwa moja langoni.

Baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa leo nahodha wa mchezo wa leo Deus Kaseke amesema kilichowaponza kufungwa ni kukosa umakini.

Kaseke amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inatafuta matokeo hivyo kushindwa kwao kupata matokeo ni sehemu ya matokeo na wanajipanga kwa ajili ya mchezo ujao.

Azam anaongoza kundi B akifuatiwa na Malindi wote wakiwa na Pointi nne, Yanga anashika nafasi ya tatu akiwa na pointi tatu, KVZ nafasi ya nne akiwa na pointi nne na nafasi ya tano inashikwa na Malindi ikiwa na pointi moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post