Klabu ya soka ya Yanga inatarajia kuwakosa viungo wake muhimu, Papy Tshishimbi na Feisal Salum 'Fei toto' katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya African Lyon utakaopigwa kesho.
Fei toto ataukosa mchezo wa kesho katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kutokana na kupewa kadi tatu za njano ambapo hivi sasa atasubiri mchezo unaofuata.
Ukiachana na Fei toto, pia inaelezwa kuwa kiungo fundi kutoka nchini Congo, papy Kabamba Tshishimbi amerejea kwao baada ya kupatwa na msiba wa baba mkwe wake hivi karibuni.
Kukosekana kwa viungo hao wawili kunafanya idadi ya wachezaji watakaokosekana katika mchezo huo kufikia wanne baada ya Andrew Vicent na Raphael Daudi kuwa majeruhi.
Yanga itavaana na African Lyon ambayo imeamua kutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama uwanja wake wa nyumbani mpaka mwisho wa msimu huu. Mpaka sasa ina pointi 44 baada ya kucheza michezo 16 huku ikiwa inaongoza ligi.