WATU WATATU WAUAWA KWA KUCHINJWA DODOMA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, amethibitisha kutokea kwa tukio la mauaji ya watu watatu wa familia moja, ambao miili yao ilibainika kuwa wameuawa kwa kuchinjwa.

Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda Muroto amesema ni kweli tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mayamaya kitongoji cha Zamahelo, na kwamba jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.

“Ni kweli tukio hilo limetokea na limetokea usiku, na watu hao baada ya kukagua miili yao ilikuwa wameuawa kwa kuchinjwa, aliyefanya tukio hajajulikana ni nani na kwanini, kama ni ugomvi tu, au walikuwa wanadaiana bado haijajulikana, jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi, ili kuweza kuwatia nguvuni wote waliohusika na tukio hilo”, amesema Kamanda Muroto.

Mauaji hayo yametokea usiku wa Desemba 13, ambapo watu watatu wa familia moja ambao ni baba aliyejulikana kwa jina la Daudi Isaya na mkewe, Hilda Mazengo na mtoto wao mchanga.

Watu hao waligunduliwa na watoto wao wakubwa baada ya kurejea nyumbani asubuhi kutoka nyumba ya jirani ambako huwa wanalala, na kukuta mlango wa wazazi wao uko wazi kitu ambacho sio kawaida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post