Saturday, December 1, 2018

RAIS MAGUFULI AWAGEUKIA WANAOCHONGANISHA NCHI

  Malunde       Saturday, December 1, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewataka mawaziri wake kujenga tabia ya kutembeleana na mawaziri wa Kenya kwa ajili ya kupatiana uzoefu kwenye masuala mbalimbali ili kuinua uchumi wa nchi hizo mbili.

"Kuna watu wengine wanachomeka maneno ya ajabu ajabu washindwe na walegee sisi tuko imara kwa ajili ya kujenga mahusiano yetu", amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizindua kituo cha huduma cha forodha kilichopo mpaka wa Namanga mkoani Arusha ambapo aliambatana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, kwenye kituo hicho ambacho kinalenga kuwawezesha wananchi waishio kwenye mpaka huo kufanya biashara kirahisi.

"Niwaombe mawaziri wa pande mbili mujenge mazoea ya kutembeleana kwa sababu Kenya ni ndugu zetu", amesema Rais Magufuli.

"Tuimarishe umoja wetu, biashara ni kati ya wananchi na Kenya na Tanzania muungane kwa kufanya biashara ya pamoja na musiwe chanzo cha kukwamishana wenyewe kwa wenyewe kupitia mpaka huu", ameongeza Rais.

Kwa upande wake Rais wa Kenyata amesisitiza juu ya umoja wa nchi hizo mbili na kudai bila kufanya hivyo, Tanzania na Kenya zitakuwa masikini.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post