TANZANIA NA UGANDA ZAKUBALIANA KUIMARISHA BIASHARA NA UCHUMI

Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.

Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula, Uganda

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527