TETESI ZA SOKA LEO BARANI ULAYA

Beki wa kulia wa Manchester United Antonio Valencia, 33, huenda akajisajiliwa na West Ham msimu ujao. (Sun)

Meneja wa Derby Frank Lampard amethibitisha kuwa Liverpool wanaweza kumchukua mshambuliaji wao wa zamani Harry Wilsoncan, 21, ambaye amekuwa akiichezea Derby kwa mkopo kufikia Januari. (Talksport)

Fulham wanapania kumsajili mlinzi wa Manchester United Matteo Darmian, 29, lakini kiungo huyo anatafakari kurudi nyumbani, kuna tetesi kuwa Inter Milan na Lazio wanammezea mate. (Tuttomercato, via Talksport)

Wolves wanajiandaa kumpatia ofa ya euro milioni 17 winga wa Japan Shoya Nakajima,24, kutoka klabu ya Portimonense ya Ureno. (Daily Mail)

Meneja wa Newcastle boss Rafael Benitez anaazimia kumsajili mshambuliaji wa Atlanta United Miguel Almiron, 24, na huenda kiungo huyo akaichezea Newcastle kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 24, huenda akahama klabu hiyo endapo hatajumuishwa katika kikosi cha kwanza mara kwa mara.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527