TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA JUMANNE DEC 11, 2018


Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 27, tena amezungumzia kuhama kwenda Real Madrid na anasema kuwa hajui ni lini ataamua hatma yake. Lakini Mbelgiji huyo amekiri kuwa mazungumzo kuhusu mkataba mpya huko Stamford Bridge yamekwama. (RMC Sport via Express)

Mkurugenbzi wa michezo wa AC Milan Leonardo amethibitisha kuwa klabu hiyo ya Serie A imezungumza Chelsea kuhusu uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31. (London Evening Standard)

Tottenham wamejiunga na Manchester United katika kumwinda mshambuliaji raia wa Romania Dennis Man, mchezaji huyo mwenye miaka 20 aiyechezea FCSB ambayo awali ilikuwa inajulikana kama Steaua Bucharest. (Sun)

Spurs wanachelewa zaidi kuufungua uwanja wao mpya kutokana na ugumu wa kuandaa warsha wakati huu wa msimu wa krismasi. (Times)

Meneja wa Fulham Claudio Ranieri yuko tayari kumsaini mchezaji wa pili Islam Slimani mwezi Januari. Ranieri alimsaini mchezaji huyo wa miaka 30 raia wa Algeria wakati akiwa meneia wa Foxes. (Telegraph)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Wolves mreno Ruben Neves anatakana mchenzia huyo mwenye miaka 21 kuhamia Juventus. (Calciomercato - in Italian)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionRuben Neves

Baba yake Miguel Almiron amesema Newcastle wako nafasi nzuri ya kumsaini mtoto wake huyo mwenye miaka 24 kutoka Atlanta United mwezi Januari. (Newcastle Chronicle)

Leeds na Aston Villa watajaribu kumsaini kipa Karl Darlow mwezi ujao. Mchezaji huyo mwenye miaka 28 alipoteza nafasi yake huko Newcastle na amecheza mechi moja peke yake msimu huu. (Sun)

Mlinzi wa zamani wa England na BT Sport pundit Rio Ferdinand alimtaja mlinzi wa Manchester City mwenye miaka 28 Kyle Walker kuwa tegemeo kubwa wakati City walishindwa na Chelsea siku ya Jumamozi kwa mabao 2-0. (Independent)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionKyle Walker

Mlinzi wa zamani wa Cardiff Greg Halford, 34, amekuwa akifanya mazoezi na West Brom na atapewa mkataba wa muda mfupi na klabu hiyo. (WalesOnline)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kuwa hataifunza Italia hivi karibuni na kupuuza maswali kuwa Nopoli wanataka huduma zake wakati akiwa huko Dortmund. (Liverpool Echo)

Wing'a wa Bayern Munich Mholanzi Arjen Robben, 34, anasema atastaafu ikiwa ofa ya sasa haitafanikiwa wakati mkataba wake utamalizika msimu huu. (Goal)

West Bromwich Albion wanataka kumsaini kuiungo wa kati wa Leicester na Wales Andy King, 30, kwa mkopo mwezi Januari. (Mail)

Chelsea watamuuza Victor Moses mwezi ujao huku Crystal Palace na Fulham wakitaka kutoa ofa zao kwa mchezaji huyo anayewekewa thamani ya pauni milioni 12 mwenye miaka 27 ambaye mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Nigeria. (Sun)

Barcelona wanamfuatilia mshambualjia wa Everton raia Brazil Richarlison, 21. (Star)

Kiungo wa kati wa kisosi cha Manchester City cha chini ya miaka 21 Phil Foden, 18, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka sita. (Telegraph)

Chelsea wanataka kumuongezea mkataba wa miaka 12 mlinzi raia wa Brazil David Luiz, 31, baada ya msimu huu ambao utamwezesha kutafuta kwingine. (Mirror)

Mlinzi wa kikosi cha chini ya miaka 21 wa Everton raia wa England Mason Holgate, 22, ameambiwa kuwa anaweza kuondoka kwa mkopo mwezi Januari. (Mirror)

Marseille wanawatafuta mabeki wawili - Nacho Monreal, 32, wa Arsenal na Alberto Moreno, 26 wa Liverpool wakati wanapanga kuboresha kikosi chao mwezi Januari. (France Football, via Mirror)

Chanzo: Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post