SCANIA TANZANIA YAZINDUA KIZAZI KIPYA CHA MALORI RAFIKI WA MAZINGIRA 'NEW GENERATION'


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika uzinduzi wa kizazi kipya cha malori ya Shirika la Scania Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa wageni kutoka mataifa mbali mbali.
Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg akizungumza katika uzinduzi wa kizazi kipya cha malori ya Shirika la Scania Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa wageni kutoka mataifa mbali mbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi akisalimiana na wageni waliohudhuria katika uzinduzi wa kizazi kipya cha malori ya Shirika la Scania Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa wageni kutoka mataifa mbali mbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Tanzania Bw. Lars Eklund akizungumza katika uzinduzi wa kizazi kipya cha malori ya Shirika la Scania Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa wageni kutoka mataifa mbali mbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba akiwa ndani ya gari ili kuona jinsi lilivyotengenezwa kwa ustadi wa aina yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba (wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa Shirika la Scania Tanzania mara baada ya kumaliza uzinduzi wa malori ya kisasa kwa kizazi kipya ambayo ni rafiki kwa mazingira (New Generation).

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Shirika la Scania Tanzania limezindua kizazi kipya cha malori kwenye sekta ya usafiri nchini huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano January Makamba akilisifu shirika hilo kwa kuzindua malori hayo ambayo ni marafiki wa mazingira.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo wa kizazi kipya cha malori ambayo mbali ya kuwa rafiki wa mazingira yemetengenezwa katika mfumo wa kuhakikisha dereva anakuwa salama hata inapotokea ajali pamoja na ulaji mdogo wa mafuta, Makamba amesema analipongeza Shirika la Scania Tanzania kwa kutambua dhana ya kutunza mazingira ambapo imeamua kuja na malori ambayo mfumo wake ni rafiki wa mazingira.

"Huko tunakoelekea iko haja ya kuhakikisha tunakuwa na vyombo vya usafiri ambavyo vitakuwa rafiki wa mazingira badala ya kuwa usafiri ambao unaharibu wa mazingira. Kuna baadhi ya vyombo vya usafiri vinatoa moshi mwingi ambao ni hatari kwa mazingira yetu, hivyo lazima tuwe na usafiri rafiki katika kuhakikusha tunakuwa salama zaidi,"amesema Makamba.

Pia Makamba amesema dunia ikiwa ni pamoja na Tanzania inakaribia hatua ya kusonga mbele ambapo kuunganishwa kwa teknolojia mpya na mifano mbalimbali ya biashara inaleta ufumbuzi wa usafiri wa kudumu na utaondoa usafiri wa kawaida.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Lars Eklund amesema Tanzania haina usafiri ambao hupunguza athari kwenye mazingira na itafanya hivyo kwa kuboresha ufanisi ambao utatoa faida za kiuchumi , kwasababu hiyo pia ni motisha kwa kila biashara." Kwa maneno mengine itaboresha afya salama katika mazingira kwa wakati mmoja."

Pia amesema kuwa ustawi wa pia ni usalama wa barabarani , hivyo wanahitaji kupunguza ajali kwa manufaa ya binadamu , kwa jamii na kwa manufaa ya biashara , mambo hayo daima huenda kwa mkono kwa mkono na faida ya ustawi na kwamba lori hiyo mpya inatoa msaada kwa dereva kikamilifu kumsaidia dereva kuendesha kwa usalama na ufanisi zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527