Utafiti : KUMPAPASA PAPASA 'KUMSHIKA SHIKA' KUNAPUNGUZA MAUMIVU

Kumpapasa papasa mtoto au kumkanda taratibu kunapunguza pakubwa shughuli katika ubongo wake hasa zinazohusiana na maumivu, utafiti umebaini hilo.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Oxford kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha John Moores cha Liverpool, ulifuatilia shughuli za ubongo wa zaidi ya watoto 32, wakati walipokuwa wakitolewa na kupimwa damu.

Nusu yao walipapaswa papaswa na brashi nyororo iliyowekwa mkononi na walionyesha asilimia 40% ya kutokuwa na maumivu kwenye bongo zao.

Mwaandishi vitabu Rebeccah Slater anasema kwamba: "Kumkanda, kumshika au kumpapasa taratibu kuna nguvu na uwezo wa ajabu, na hauna madhara ya pembeni kabisa."

Utafiti huo aidha umebaini pia kuwa, kasi ya kupunguza machungu ni kama sentimita 3 kwa sekunde moja.

"Mara nyingi wazazi huwapapasapapasa watoto wao katika kasi ya kawaida tu," anasema Prof Slater.

"Ikiwa tutaelewa kinachofanyika ndani ya viungo vya mwanadamu hasa mawasiliano ya ubongo pamoja na mbinu za kupasha ujumbe wa kimya ndani ya watoto, tunaweza kuboresha zaidi mashauri ambayo tunawapa wazazi ili kuliwaza watoto wao."

Shughuli za mwendo kasi za kumliwaza mtoto kwa kumpapasa papasa, huzindua aina fulani ya niuroni iliyo na hisia katika ngozi aitwaye C-tactile afferents, ambayo inaonekana kupunguza maumivu kwa watu wazima.

Lakini haikuwa wazi, iwapo watoto wana mwitikio sawa au hukuwa kadri muda unavyokwenda.

"Kuna ushahidi unaoonyesha kuwa, hisia iitwayo C-tactile afferents, inaweza kuzinduliwa ndani ya watoto, na mguso huo wa upole na taratibu, unaweza kuleta mabadiliko makubwa mno kwenye ubongo wa watoto," anasema Prof Slater.
Prof Slater anasema utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la Current Biology, na kuelezea ushahidi wa kina na wa nguvu wa mguso ambao umo chini ya mfuko wa kumbebea mtoto maarufu kangaroo care, mahali ambapo watoto ambao wamezaliwa kabla ya muda wao kufika. Sasa wazazi wanashauriwa kuwapa mguso, kupapasa au kuwakanda wana wao katika harakatai za kupunguza machungu ambayo wanaweza kuyapitia baadaye maishani.

"Kazi za awali zimeonyesha bayana kuwa, mguso unaweza kuongeza uhusiano wa karibu mno kati ya mtoto na mzazi, kupunguza shinikizo la moyo kwa mzazi na mtoto, na kupunguza muda mrefu wa kusalia Hospitali," anaongeza Prof Slater.

Waandishi wa uchunguzi huo sasa wana mpango wa kurudia zoezi hilo kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa kufika, na ambao bado baadhi ya sehemu ya viungo vyao hasa sehemu zao za mwili zinazohusiana na kuhisi zinaendea kukuwa.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Bliss lisilokuwa la kiserikali, na ambalo linalowashughulikia watoto wagonjwa nchini Uingereza, Caroline Lee-Dave , amesifia sana utafiti huo.

Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post