MWANAMKE MBARONI KWA KUJIFANYA MJAMZITO KISHA KUBEBA MIRUNGI KUTOKA TARIME

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kutumia kikosi chake kabambe chenye uweledi wa hali ya juu na uaminifu uliotukuka tumefanikiwa kuwakamata watu wa nne kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya mirungi kiasi cha kilo gramu 18. 

Ambapo mtuhumiwa mmoja alikamatwa kwenye bus maeneo ya Nyakato akiwa anasafirisha mirungi toka Tarime kuja Mwanza na wengine watatu walikamatwa huko mtaa wa Mahina Wilayani Nyamagana, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Watuhumiwa hao wamekamatwa tarehe 09/12/2018 majira ya saa 20:00hrs, hii ni baada ya kupatikana kwa taarifa toka kwa raia wema kwamba huko mtaa wa mahina yupo mtu anayefanya biashara ya dawa za kulevya aina ya mirungi ndipo askari tulifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na mirungi kiasi cha kilogramu 10.

Watuhumiwa hao waliokamatwa wamefahamika kwa majina yafuatayo;
  1. Saad Saba Kapinga, miaka, 49, mkazi wa mahina
  2. Fatiha Saba, miaka 15, mwanafunzi wa kidato cha tatu Thaqaafa secondary.
  3. Karen Saba, miaka 13, mwanafunzi wa kidato cha pili Musabe secondary.
Vilevile Mtuhumiwa mwingine mwanamke aitwaye Frola Mwita miaka 40, mkazi wa tarime alikamatwa na mirungi kiasi cha Kilogramu 8, alizokuwa amezifunga tumboni kwa seal tape na kuonekana kama mwanamke mjamzito akisafirisha na bus la Zacharia lenye namba T.569 CAP toka Tarime kuja Mwanza .

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote wa nne pindi uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani. 

Pia msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wa mtaa mahina ambao wamefanikiwa kutoroka bado unaendelea. Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunaendelea na msako na ukaguzi wa magari yote yanayoingia Jijini Mwanza toka maeneo mbalimbali.

Katika tukio la Pili
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kutumia kikosi chake makini chenye uweledi wa hali ya juu tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu  ishirini na saba (27) toka nchi ya DRC –CONGO, walioingia Nchini bila kibali huko kwenye kivuko cha Busisi /Kigongo Ferry Wilayani Sengerema, kitendo ambacho ni kosa la Jinai.

Operesheni hiyo kabambe iliyofanikisha kukamata wahamiaji hao haramu imefanyika tarehe 09.12.2018 majira ya saa 22:00hrs usiku, wakati askari tukiendelea na doria pamoja na msako mkali katika kivuko cha Busisi ndipo tulipokea taarifa toka kwa wasiri kwamba lipo gari kivukoni hapo limebeba wahamiaji haramu.

Baada ya kupokea taarifa hizo, Polisi tulifanya msako mkali  pamoja na ukaguzi wa magari yote yaliyokuwepo kivukoni hapo na kufanikiwa  kuwakamata wahamiaji hao haramu ishirini na saba (27) wakiwa ndani ya gari wakielekea Jijini Mwanza, kati yao wanaume ni 15 na wanawake ni 12.

Wahamiaji hao haramu wamefahamika   kwa majina yafuatayo;
  1. Luganga Feruzi, miaka 40, toka jimbo la Kivu ya kusini Nchini DRC –Congo.
  2. Maria Ramadhani, miaka 30,  toka Jimbo la Kivu ya kusini Nchini DRC –Congo.
  3. Hamis  Luganga, miaka 12, mwanafunzi wa darasa la sita, Nchini DRC –Congo
  4. Hatia Lugunga, miaka  5, toka Nchi DRC –Congo
  5. Kyala  Lugunga, miaka  09 mwanafunzi wa darasa la tatu Nchini DRC- Congo
  6. Byaombe  Lugunga,mwanafunzi wa darasa la kwanza Nchini DRC –Congo
  7. Wilonja  Lugunga, miaka 5, toka Nchini DRC –Congo
  8. Ramadhan  Lugunga , miaka 3, toka Nchini DRC- Congo
  9.  Wilonja  Etungano, miaka 35, toka Kivu ya Kusini Nchini DRC – Congo
  10. Mitamba Ilonja, miaka 33, toka Kivu ya kusini Nchini DRC –Congo
  11. Byaombe Wilonja, miaka 16, mwanafunzi wa darasa la nne Nchini DRC- Congo
  12. Jilibeye Wilonja, miaka 13, mwanafunzi wa darasa la pili Nchini DRC –Congo.
  13. Mwenge Wilonja , miaka 12, Mwanafunzi wa darasa la nne Nchini DRC –Congo.
  14. Lucia Wilonja, miaka 10, mwanafunzi wa darasa la pili Nchini DRC –Congo.
  15. Joro Wilonja, miaka 8, mwanafunzi wa darasa la kwanza Nchini DRC –Congo.
  16. Shansi Wilonja, miaka 4, toka Nchini DRC – Congo
  17. Saidi Wilonja, miaka  2, toka Nchini DRC- Congo.
  18. Mbekalu  Asikulu, miaka 31, toka jimbo la Kivu ya Kusini Nchini DRC –Congo.
  19. Hamis Venance, miaka 30, toka jimbo la kivu ya Kusini Nchini DRC –Congo
  20. Maselina Mwibelecha, miaka 23, toka jimbo la Kivu ya Kusini Nchini DRC – Congo.
  21. Kashindi Hussein, miaka 3, toka jimbo la Kivu ya kusini Nchini DRC – Congo.
  22. Salive Hussein, mwaka 1, toka Nchini DRC –Congo.
  23. Regina Maua, miaka 28, toka  Jimbo la Kivu ya Kusini Nchini DRC –Congo.
  24. Debora Jamali, miaka 12, mwanafunzi wa darasa la nne Nchini DRC –Congo.
  25. Joseph Jamali, miaka 8, mwanafunzi wa darasa la pili Nchini DRC –Congo.
  26. Malekesa Jamali, miaka 5, toka Nchini DRC –Congo.
  27.  Jackson Jamali, miaka 2, toka Nchini DRC –Congo.
Aidha sababu za wahamiaji hao haramu kukimbia Nchini mwao DRC –Congo bado hazijafahamika. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunaendelea na uchunguzi pamoja na mahojiano na wahamiaji hao haramu ili kuweza kufahamu sababu zilizowafanya kukimbia Nchi yao ya DRC –Congo. Lakini pia kuweza kubaini mbinu walizotumia kuingia Tanzania bila ya kukamatwa hadi kufika Mwanza. Aidha pindi uchunguzi ukikamilika wahamiaji hao haramu watakabidhiwa Idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kuwa waache kwani ni kosa la Jinai na endapo mtu atabainika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 

Sambamba na hilo tunaendelea kuwaomba wananchi kuendelea kutupa ushirikiano kwa kutupa taarifa za wakimbizi/wahamiaji haramu wanaongia Nchini bila kufuata sheria ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527