MOYO WASAHAULIKA KWENYE NDEGE,YALAZIMIKA KUKATIZA SAFARI YAKE

Ndege ya abiria ya Marekani iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Seattle kuenda Dallas ililazimika kukatiza safari baada ya moyo wa binadamu kusahaulika ndani yake.

Shirika la ndege la Southwest linasema kuwa kiungo hicho kilisafirishwa Seattle kutoka California, ambako ilitarajiwa kutolewa mishipa ambayo ingetumiwa baadaye kwa utaratibu wa tiba ya upandikizaji.

Lakini kisanduku ambacho kilikuwa kimehifadhi moyo huo kilisahaulika ndani ya ndege hiyo na hilo lilifahamika baada ya ndege kuanza safari kuelekea Dallas.

Kisa hicho kilitokea siku ya Jumapili lakini kiliangaziwa katika vyombo vya habari siku ya Alhamisi.

Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanasemakana kushutuka sana wakata rubani alipowaambia kuhusiana na mzigo huo na kwamba hana budi kugeuza mkondo na kurejea walikotoka.

Baadhi yao walitumia simu zao kujifahamisha kuhusu muda ambao moyo unaweza kuhifadhiwa kabla ya itumike kwa upasuaji- kwa mujiu wa wataalamu, moyo wa binadamu huchukuwa kati ya saa nne na sita kuharibika.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post