MBOWE ATUMA UJUMBE KUTOKA GEREZANI


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad, ameweka wazi mipango ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe baada ya kutoka gerezani ni kuungana na vyama vingine vya upinzani.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo baada ya kutumia siku ya Jumamosi ya leo kuwatembelea viongozi Mwenyekiti Mbowe pamoja na Mbunge Esther Matiko katika gereza la Segerea baada ya kufutiwa dhamana.

"Nimeitumia fursa ya kuonana na Mhe. Freeman Mbowe na Mhe. Esther Matiko kuwaeleza kuhusu Azimio la Zanzibar na mikakati ya vyama sita vya siasa kurudisha demokrasia Tanzania. Mhe. Mbowe amenambia yuko pamoja na sisi na akitoka tu gerezani ataungana nasi kuendeleza atakapopakutia" Amesema Maalim Seif

Aidha kiongozi huyo amebainisha kwamba viongozi hao wawili bado wapo imara na wana imani kwamba haki itatendeka juu yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527