MAHAKAMA YA MAFISADI TANZANIA YAMTUPA JELA MAISHA RAIA WA ETHIOPIA

Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi ‘Mahakama ya Mafisadi’ imemuhukumu kifungo cha maisha jela raia wa Ethiopia, Ana Moises Chissano baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine Kg 3.03.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Lilian Mashaka ambapo amesema mshtakiwa huyo amefungwa chini ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.


Mahakama imeamuru dawa hizo ziteketezwe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post