MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MFANYABIASHARA ALIYETUHUMIWA KUMPA RUSHWA LUKUVI

Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemuachia huru mfanyabiashara, Mohamed Kiluwa (50) baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Kiluwa alikuwa anakabiliwa na shtaka moja la kutoa rushwa ya dola za kimarekani 40,000 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Desemba 24, 2018 na Hakimu Mkazi, Samuel Obasi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutolewa hukumu.

"Ushahidi wa upande wa mashtaka umekaa kihisia zaidi, hivyo mahakama yangu imeshindwa kumtia hatiani mshtakiwa, hivyo mahakama hii imemuachia huru Kiluwa" amedai Hakimu Obasi na kuongeza: "Hisia hata kama zina nguvu kiasi gani, haziwezi kufanya mahakama imtie hatiani," amesema Hakimu Obasi.

Na Hadija Jumanne, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527