MWANAMKE ABAKWA NA WANAUME WAWILI KISHA KUCHOMWA MOTO

Mwanamke mmoja kaskazini mwa India yupo katika wodi ya wagonjwa mahututi hali mbaya baada ya kuchomwa moto na wanaume wawili ambao inasemekana walimbaka.

Mkasa huo wa kuchomwa moto umetokea wakati mwanamke huyo akiwa njiani kufungua kesi ya malalamiko polisi siku ya Jumamosi.

Inaripotiwa kuwa awali polisi waliwahi kataa kumpa ushirikiano.

Washukiwa wote wamekamatwa na polisi watatu wamesimamishwa kazi, afisa wa polisi ameiambia BBC.

Mwanamke huyo kwa sasa anamajeraha makubwa ya moto.

Wanaharakati wanasema swala la polisi kunyanyasa watu waliobakwa si jambo jipya. Na kesi nyingi za ulawiti, ubakaji na utumwa wa kingono haziripotiwi polisi huko India kutokana na mitazamo hasi juu ya ubakaji lakini pia hali ya polisi kutokujali.

Shambulizi hilo kwa mwanamke wa miaka 22 limefanyika katika wilaya ya Sitapur kwenye jimbo la Uttar Pradesh.

Tarehe 29 mwezi Novemba alibakwa na ndugu wawili ambao ni mtu na kaka yake katika uwanja wa mpira jirani na nyumbani kwao.

Alifanikiwa kuwakimbia na kwenda katika kituo cha polisi akisindikizwa na baadhi ya ndugu ili kufungua mashitaka. Lakini familia yake imesema kuwa hawakusikilizwa na polisi.

Siku ya jumamosi, siku mbili tangu alipobakwa, aliamua kwenda polisi ili kujaribu tena kufungua mashitaka ambapo washitakiwa walimwagia mafuta ya taa na kumchoma moto akiwa njiani, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Afisa mmoja wa juu wa polisi amewaambia waandishi wa habari wanachunguza ili kujua ni kwa nini maafisa waliokuwepo zamu hawakufungua kesi ya malalamiko ya awali.

Amesema watuhumiwa wote wawili na polisi wawili wa zamu wamesimamishwa kazi kwa kudharau majukumu yao.

Wasichana watatu walibakwa na kuchomwa moto wakiwa hai katika matukio tofauti na mikoa tofauti mwaka huu pekee nchini India. Wawili walifariki kutokana na majeraha.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post