BILIONI 133.2 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa mpaka kufikia jana tarehe 14 Disemba 2018 wakulima 130,163 wamelipwa jumla ya shilingi 133,259,933.855


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa takwimu hizo tarehe 15 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.


Alisema kuwa katika Mkoa wa Mtwara wananchi ambao wamekwishalipwa ni 77,055 huku jumla ya fedha iliyolipwa ni Bilioni 80,098,982,060 


Katika mkoa wa Lindi tayari wakulima 41,564 wamekwishalipwa kiasi cha Bilioni 42,502,635,227 huku katika mkoa wa Ruvuma wakulima 11,463 wamekwishalipwa kiasi cha Bilioni 10,557,222,943


Aidha, Mhe Hasunga amesema kuwa katika mkoa wa Pwani Milioni 101,091,960 zimekwishalipwa kwa wakulima 81


Alisisitiza kuwa vyama vilivyohakikiwa ni 461 na vilivyolipwa ni 451, ambapo jumla ya Kilo 40,381,798

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post