AJIUA YEYE NA WATOTO WAKE KWA MOTO, KISA MKE WA PILI

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26, Rukia Wasuna mkazi wa Kaunti ya Kisumu nchini Kenya, ameamua kujiua yeye pamoja na watoto wake, baada ya mume wake kumwambia kuwa anataka kuoa mke wa pili.

Tukio hilo ambalo limetokea Jumatatu ya Desemba 10, 2018 huko Otonglo Kisumu, limethibitishwa na chifu wa eneo hilo, Osege Orwa ambapo amesema mwanamke huyo alijiua kwa moto, aliouwasha mwenyewe kwenye nyumba baada ya kujifungia ndani yeye pamoja na watoto wake wawili, mmoja akiwa na miaka 6 na mwingine mwenye miaka mitatu.

Akielezea kwa undani zaidi tukio hilo, Chief Orwa amesema kwamba wamepata taarifa kuwa mume wa mwanamke huyo alikusudia kuoa mke wa pili, sababu ambayo ilipelekea mwanamke huyo kununua petroli na kuimwagia nyumba, kisha kujifungia yeye na watoto wake, na kuichoma moto ambao uliwateketeza.

Wakati tukio hilo linatokea, mume wa marehemu alikuwa kazini kwake katika eneo la Eldoet, na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post