DIAMOND PLATNUMZ ATANGAZA NDOA NA NATASHA

Baada ya kuachana na Zari, kwa sasa Diamond ameweka majeshi kwa mrembo wa Kenya, ambaye ni mtangazaji wa Kituo cha Luninga cha NRG, aitwaye Natasha.

Diamond inaelezwa kuwa amepagawa na penzi la Tanasha Donna kwa sasa anawaza ndoa tu.

Wiki iliyopita Diamond alifanya show mjini Thika na Tanasha alikuwepo na hapo akatambulishwa rasmi kwa mashabiki kwamba, ndiye mpango mzima kwa sasa.


Pia, Diamond aliweka bayana kwamba, miongoni mwa wasichana aliowahi kuwa nao amemwelewa zaidi Tanasha hivyo, anataka kufuta rekodi zote za nyuma na kutulia na mrembo huyo.


“Tanasha ndiye mwanamke pekee aliyeonesha kujali na uzito juu ya jambo hilo hivyo rasmi natangaza kumuoa huyu. Ana sifa zote za mwanamke wa kuoa, lakini unajua sisi wanaume wengi huwa tunaangalia sura, umbo na vingine vya mwilini kisha ndiyo inafuata tabia. Lakini nimejiridhisha kwamba mbali na umbo na mvuto wa kipekee pia ni mwanamke mwenye tabia nzuri,” Diamond alikiambia chombo kimoja cha habari nchini Kenya alikokuwa wiki iliyopita kwaajili ya show.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527