Tuesday, December 4, 2018

BENKI YA CRDB YAPATA DAKTARI MPYA

  Malunde       Tuesday, December 4, 2018

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Mwanza, Danford Muyango (pichani) ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo Kikuu cha Dodoma “UDOM” na hivyo kuwa daktari mpya kwa sasa anayefanya kazi na benki hiyo.

Sasa atafahamika kama “Dkt. Danford Muyango” akiwa ni miongoni mwa vijana wachachenchini waliofikia hatua hiyo kielimu. Dkt. Muyango amehitimu Ndaki ya Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii akibobea kwenye fani ya taasisi ndogondogo za fedha na maendeleo ya wanawake.

Dkt. Muyangoalitunukiwa shahada hiyo Novemba 23, 2018 na Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM ambaye pia ni Rais Mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Mhe. Benjamin Willium Mkapa.

“Namshukru Mwenyezi Mungu pamoja na wale wote waliotoa mchango wao wa hali na malikuhakikisha nafikia hatua hii, hivyo ni wajibu wangu sasa kuendelea kuitumikiajamii kwa ari kubwa”. Alisema Dkt. Muyango.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Dkt. Danford Muyango (kushoto), akitunukiwa Digrii ya tatu ya Uzamivu (PhD), na Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM Mhe. Benjamin Mkapa kwenye mahafali ya tisa ya chuo hicho yaliyofanyika Novemba 23, 2018. Dkt. Muyango amehitimu Ndaki ya Sanaa, Lugha na Sayansi ya Jamii akibobea kwenye fani ya taasisi ndogondogo za fedha na maendeleo ya wanawake.
Dkt. Danford Muyango akiwa kwenye mahafali ya tisa ya Chuo Kikuu cha UDOM yaliyofanyika Novemba 23, 2018 Jijini Dodoma.
Dkt. Danford Muyango (kushot), akiwa na Msimamizi "Supervisor" wake wa PhD, Dkt. Rehema Kilonzo (kulia).
Dkt. Danford Muyango (kulia) akiwa pamoja na baba yake mzazi, Mzee Muyango.
Dkt. Danford Muyango akiwa pamoja na wanafamilia.
Dkt. Danford Muyango akiwa na mkewe Neema Muyango pamoja na watoto wake Davina na Delvin
Dkt. Danford Muyango (kulia) akiwa na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Chabu Mishwaro (kushoto).
Dkt. Danford Muyango (kushoto) akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM, Utafiti, Taaluma na Ushauri Profesa Msofe (kulia).
Dkt. Danford Muyango (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post