RAIS MAGUFULI ASHANGAA UFUKWE WA COCO BEACH KUKOSA CHOO

Rais John Magufuli ameshangazwa na ufukwe wa Coco (Coco Beach) pembezoni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam kutokuwa na choo wakati eneo hilo zinakusanywa fedha kila siku.


Akizungumza leo Alhamisi Desemba 20, 2018 kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Selander jijini Dar es Salaam, Rais amedai magari yanayoegeshwa kando ya fukwe hiyo hulipiwa Sh2,000.

“Coco Beach panatia aibu. Ifike wakati tuzizungumzie aibu zetu pale hakuna hata choo, ndio nasikia wanajenga sasa,” amesema.

“Wanakusanya mapato kila siku hatujui hizo hela zinakwenda wapi na wanashindwa hata kujenga mabanda yaliyoboreshwa.”

Hata hivyo, amesema Jiji la Dar es Salaam limebadilika na kuwa na sifa ya kuwa jiji la kibiashara, kwamba anafurahi kuhamia Dodoma akiacha Dar es Salaam ikiwa katika hali hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post