AJALI ZA BARABARANI ZAUA ZAIDI YA UKIMWI BARANI AFRIKA

Ajali za barabarani zinatajwa kuwa ndio zinasababisha vifo vingi vya watoto na vijana duniani, kwa mujibu wa shirika la afya duniani(WHO).

Shirika hilo la afya limechapisha ripoti ambayo inabainisha kwamba bara la Afrika ndilo lina ajali nyingi za barabarani duniani.

Katika taarifa nyingi zinasema kwamba waafrika na wamarekani wa Kusini bado hawana sheria nzuri za kudhibiti mwendo kasi.

Lakini taarifa hizo zimesisitiza kwamba vifo vinavyotokana na ajali za barabarani duniani huwa zinalingana na kiwango cha idadi ya watu.

Ajali za magari ndio zinaongoza duniani kusababisha vifo kwa watoto na vijana wenye umri kati ya miaka mitano mpaka 29, ripoti hiyo imesema.

Ripoti hiyo pia imeeleza kwamba watu wengi zaidi wanakufa kutokana na ajali za barabarani kuliko virusi vya ukimwi , kifua kikuu au magojwa ya kuhara.

"Vifo hivyo havikubaliki, hakuna sababu inayoweza kutetea matukio hayo .Hili ni tatizo ambalo linaweza kutafutiwa ufumbuzi" Mkurugenzi wa WHO alisema.

Chanzo:Bbc


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527