AFISA UHAMIAJI AFARIKI BAADA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI


Na John Walter-Babati
Afisa uhamiaji Mkoani Manyara aliyefahamika kwa jina la Peter Kambanga (35- 40) amepoteza maisha usiku wa alhamisi Disemba 27 kwa kile kinachoelezwa kunywa pombe kupita kiasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Agustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi hilo lilifika katika chumba alichopanga marehemu, mjini Babati na kukuta kimefungwa kwa ndani na kuwalazimu kuvunja ndipo walipoukuta mwili huo.

Kamanda Senga amesema kuwa chanzo cha kifo hicho ni unywaji wa pombe kupindukia na kukosa hewa na kuongeza kuwa alikuwa akiishi mwenyewe katika chumba alichokuwa amepanga.

Aidha Senga amesema mwili wa Marehemu umesafirishwa leo Jumamosi Disemba 29,2018 kwenda wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma kwa ajili ya taratibu za Mazishi.

Kamanda Senga ametoa wito kwa wakazi wa Manyara kuishi pamoja na ndugu au familia zao pindi wanapokuwa mbali kikazi.

Sambamba na hilo jeshi la polisi mkoani Manyara limewasishi wananchi kunywa pombe kistaarabu na kuendesha magari kwa uangalifu huku likizidi kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu katika kipindi hiki cha siku kuu za mwisho wa mwaka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post