VIKUNDI 750 VYA WAKULIMA WILAYANI KISARAWE KUKABIDHIWA HATI MILIKI ZA ARDHI


Ofisa Miradi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda, akizungumza na wadau wa kilimo ambao ni wanachama wa shirika hilo kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa Jukwaa la Wakulima wilayani Kisarawe mkoani Pwani pamoja na kukabidhiwa hati miliki za ardhi. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni.
Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Ivy Jamson Mwansepe, akitoa taarifa ya shirika hilo wakati wa mkutano huo. 
Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Ivy Jamson Mwansepe, akimkabidhi taarifa hiyo Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa mkutano huo. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Nzenga, Mohammed Rubondo, Diwani wa Kata ya Mafizi, Yadhamen Nghonde, Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni, Ofisa Miradi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda na Mwenyekiti wa shirika hilo, Isabela Luoga.
Wadau wa kilimo wakiwa kwenye mkutano huo.
Ofisa Ugani kutoka Shirika la Yara Tanzania LTD, Maulidi Mkima, akizungumza kwenye mkutano huo.
Linda Byaba kutoka Kilimo Joint LTD, akizungumza.
Wadau wa kilimo wakiwa kwenye mkutano huo.
Shabani Maulidi Mataula, akichangia jambo.
Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkazi wa Kata ya Kurui, Salumu Jaza, akichangia jambo.
Mkazi wa Kijiji cha Zagero, Fatuma Mindu, akichangia jambo.
Ofisa Ugani wa Kata ya Marui, Fadhil Mkomeka, akichangia jambo.
Mdau wa kilimo, Charles Andrea Mattaka, akizungumza katika mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Nzenga, Mohammed Rubondo, akizungumza.
Diwani wa Kata ya Mafizi, Yadhamen Nghonde, akielezea kuhusu hati miliki za ardhi.

Na Dotto Mwaibale, Kisarawe

VIKUNDI vya wakulima 750 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani vinatarajia kukabidhiwa hati miliki za ardhi zitakazoweza kuwasaidia kupata mikopo katika taasisi za fedha.

Hayo yalibainika wilayani humo juzi katika Kijiji cha Zegero wakati wa mkutano wa mchakato wa kuanzisha jukwaa la wakulima unaoratibiwa na Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association kwa kushirikiana na Ofisi ya mkurugenzi wa halmshauri hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo Ofisa miradi wa shirika hilo, Said Simkonda alisema kati ya vikundi hivyo vitakavyopata hati hizo vikundi 250 ni vya watu wenye ulemavu ambavyo vimepata mashamba kwa ajili ya kufanya kilimo.

Akizungumzia kuhusu uanzishwaji wa jukwaa la wakulima alisema litakuwa ni chombo cha kuwakutanisha wakulima wote waliomo wilayani Kisarawe na mikoa ya jirani ili kuleta kilimo chenye tija.

Alisema mchakato huo umewahusisha wadau wa kilimo kutoka Kata ya Kurui, Mzenga, Mafizi, Vihingo, Marui na Chole na kuwa shirika hilo linaupongeza uongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa kulidhia kuupokea mradi huo wa kilimo mnamo mwaka 2016.

"Tangu tuanze kushirikiana na Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe shirika letu limeweza kuwasaidia wakulima ambao ni wanachama wao 255 na kuwapatia mafunzo ya kilimo na kuwa linatarajia kuendeleza kutoa mafunzo ya kompyuta, scanner, intaneti na kuendesha huduma za ugani kwa wakulima.

Alisema pamoja na mambo mengine wanatarajia kuanzisha soko la kimataifa la mazao mbalimbali wilayani humo ili mazao yote yanayolimwa wilayani humo yapatikane eneo moja kama lile la Kibaigwa.

Diwani wa Kata ya Kurui ambaye aliongoza mchakato wa kuanzishwa kwa jukwaa hilo la wakulima, Musa Kunikuni alisema jukwaa hilo ni muhimu sana kwao kwani litawasaidia kuwaweka pamoja na kuwa hizo hati miliki za ardhi wakizipata zitawasaidia kupata mikopo ya kuendeleza kilimo.

Diwani wa Kata ya Mafizi, Yadhanen Nghonde alisema ni muhimu hati hizo zikatolewa haraka ili wakulima waliowanachama waweze kujipanga kwa kuomba mikopo itakayowasaidia msimu ujao wa kilimo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527