TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI TCRA

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi na kuondoa malalamiko kutopata huduma stahiki.

Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji kwa channeli zinazotazamwa bila malipo iliyowashirikisha watendaji wa mitaa,Kata, Wakuu wa vituo vya polisi,waalimu wakuu wa shule sanjari na watumisha wa idara za serikali wilayani hapa Meneja wa mamlaka hiyo Mhandisi Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao hawana.

Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili kuweza kumlinda mlaji.

“Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka kwao ili kuweza kuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.

Kwa Upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amesema kuwa mbali na malalamiko mbali mbali yaliyotolewa na washiriki wa mkutano huo suala zima ni ushirikiano kati ya Tcra na wadau mbalimbali na semina hiyo imefungua milango kwa wananchi kwani elimu itawafikia walengwa ambao ni wananchi.

Amesema kuwa semina hiyo inatakiwa kuwa endelevu na watendaji wamejipanga kuhakikisha kuwafikishia wananchi kwenye maeneo yao na tutarajie kuondoa changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi hususani ya wizi wa mtandao.


“Natoa rai kwa TCRA kuhakikisha changamoto mbali mbali zinazoelekezwa kwao kuzitafutia ufumbuzi ili kuondoa kero na adha wanayokutana nayo wananchi katika maeneo mbali mbali hapa nchini tunashukuru sana sisi tumepata uelewa wa masuala haya ya channel zisizolipiwa na tunaahidi kutoa elimu kwa wananchi”alisema Mwakiposa


Aidha Baadhi ya washiriki mbali mbali walioshiriki katika semina hiyo wamepata uelewa ila wakaitaka Tcra kuenda mbele zaidi katika suala zima la utoaji wa elimu kwa wananchi sanjari na kutatua changamoto mbali mbali wanazokutana nazo walaji wa mamalaka hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post