TANZANIA YATOA SABABU YA KUTOSAINI MKATABA WA AFRIKA KUHUSU DEMOKRASIA, CHAGUZI NA UTAWALA BORA

Tanzania imetaja sababu za kutotia saini mkataba wa Afrika kuhusu demokrasia, chaguzi na utawala bora ikisema ni kutokana na baadhi ya vifungu kukinzana na ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Damasi Ndumbaro ameliambia Bunge hayo jana wakati akijibu swali bungeni.


Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Neema Mgaya alisema miaka sita iliyopita Tanzania ilishiriki nakupitisha azimio kuhusu masuala ya demokrasia, chaguzi na utawala bora na kutaka kujua hadi sasa Serikali imefikia wapi.


"Je Serikali inaweza kueleza ni kwa nini hadi leo azimio hilo halijaridhiwa na kusainiwa rasmi na Serikali ina mkakati gani kuhakikisha linaridhiwa?," alihoji Mgaya.


Akijibu, naibu waziri huyo alisema hadi sasa ni nchi 35 tu ndizo zimeridhia mkataba huo wakati nchi 19 hazijaridhia ikiwamo Tanzania.


Alisema wakuu wa nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika walikutana Januari 30, 2007 na kuzitaka nchi kuzingatia na kutekeleza utawala bora, utawala wa sheria na haki za binadamu kama ilivyo katika ibara ya 3 na 4 ya mkataba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527