MJUE MTAALAMU WA NYOKA ALIYEANDIKA KIFO CHAKE BAADA YA KUNG'ATWA NYOKA

Mnamo Septemba 1957, mkurugenzi wa kituo cha kuwahifadhi wanyama cha Lincoln Park Zoo mjini Chicago aliagiza nyoka mmoja atumwe kwenye Makumbusho ya Historia ya Maumbile atambuliwe ni wa aina gani.


Nyoka huyo mwenye urefu wa sentimita 76 alifaa akaguliwe na Karl Patterson Schmidt, mtaalamu maarufu wa nyoka aliyekuwa amefanya kazi katika makumbusho hayo kwa miaka 33.

Alikuwa mtaalamu wa nyoka wanaokaa kwenye matumbawe na alikuwa amejikusanyia mkusanyiko mkubwa sana wa nyoka kutoka kila pembe ya dunia kufikia wakati wa kustaaf wake kama Mhifadhi Mkuu wa Viumbe mwaka 1955.

Lakini alishangazwa na hali kwamba gamba lake la kwenye sehemu ya haja, ambalo hufunika sehemu ya kuendea haja, halikuwa limegawanyika.

Hatua aliyoichukua baada ya hapo ilimgharimu maisha yake; alimnyanyua nyoka huyo ili kumtazama kwa makini ,
alipomuinua nyoka huyo, alimshambulia na kumuuma kidole cha gumba cha mkono wake wa kushoto, na kumuacha na vidonda viwili vidogo, vilivyokuwa vinavuja damu kidogo.

Schmidt alianza kuinyonya damu kutoka kwenye kidole chake cha gumba badala ya kutafuta usaidizi wa kimatibabu,alianza kuandika kuhusu athari za sumu hiyo kwenye mwili wake.

Chini ya saa 24 baadaye, alikuwa ameshafariki.

Nyoka aliyemuua mtaalamu huyo baadaye ilibainika kwamba alikuwa aina ya Boomslang, kama huyu aliyeko pichani


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527