MOURINHO AFUNGUKA KUONDOKA KWA SANCHEZ MANCHESTER UNITED


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameweka wazi kuwa nyota wa timu hiyo Alexis Sanchez, hajaonyesha nia ya kutaka kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Sanchez ambaye alijiunga na Man United miezi 10 iliyopita akitokea Arsenal amekuwa kwenye wakati mgumu ndani ya kikosi cha Mreno Jose kutokana na kutopata nafasi mara kwa mara.

''Alexis Sanchez hajaomba kuondoka Manchester United mwezi Januari'', alijibu Jose Mourinho swali la mwanahabari mmoja kwenye mkutano kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Crystal Palacemchezo huo utakaoanza leo saa 12:00 jioni.

Mpaka sasa nyota huyo wa Chile mwenye umri wa miaka 29 amefunga bao moja tu katika michezo 11 ya ligi kuu ya England msimu huu.

Ripoti zinasema Sanchez anaweza kutafuta timu nje ya England wakati wa dirisha dogo la usajili. Lakaini Mourinho amesisitiza kuwa hajawahi kuambiwa na Sanchez kuhusu kuondoka ama mchezaji huyo kutokuwa na furaha ndani ya United.

Manchester United haijawa na matokeo mazuri msimu huu ambapo mpaka sasa ipo katika nafasi ya 8 ikiwa na alama 20 katika michezo 12. Leo watakuwa wenyeji wa Crystal Palace ambao wanashika nafasi ya 16 wakiwa na alama 8 kwenye michezo 12.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527