SADIO MANE KUBAKI LIVERPOOL MPAKA 2023, JURGEN KLOPP AMWAGIA SIFA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, November 23, 2018

SADIO MANE KUBAKI LIVERPOOL MPAKA 2023, JURGEN KLOPP AMWAGIA SIFA

  Kanyefu       Friday, November 23, 2018

Mchezaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane amekubali mkataba wa muda mrefu kuendelea kucheza Anfield.

Mchezaji huyo mwenye miaka 26 alijiunga na klabu hiyo kutoka Southampton kwa mkataba wa miaka 5 mnamo Juni 2016 kwa thamani ya £ milioni 34.

Tangu hapo amecheza mara 89 katika mashindano yote ya timu hiyo ya Jurgen Klopp na kufanikiwa kufunga magoli 40.

"Ninafurahia sana kurefusha muda wangu Liverpool. Ni siku nzuri mno kwangu na huu ni uamuzi bora kabisa katika kazi yangu," amesema.

Mazungumzo kuhusu mkataba huo unaodumu hadi 2023, yaliidhinishwa mwishoni mwa msimu uliopita lakini yamekamilishwa hivi punde tu.

"Natazamia kila kitu - kuisaidia timu, kuisaidia klabu kutimiza ndoto yetu hususan kushinda mataji," aliongeza.

"Daima nimekuwa nikisema, nilipojuwa nina nafasi kuja hapa sikufikiria mara mbili. Klabu muafaka, kwa wakati muafaka, kwa kocha aliye sawa. Nilikuja hapa na nilifurahi sana.."

Mane alipigiwa kura kuwa mchezaji bora wa timu hiyo na mchezaji bora wa wachezaji katika msimu wake wa kwanza na baadaye akafunga magoli 10 kati ya yake 20 msimu uliopita katika ligi ya mabingwa wakati Liverpool ilipofika katika fainali.

Aliichezea timu ya taifa ya Senegal katika mashindano ya kombe la dunia 2018 nchini Urusi na kufanikiwa kufunga mara moja katika mechi tatu za nje.

Hivi karibuni ametajwa katika orodha ya wachezaji 30 watakaowania  tuzo ya Ballon d'Or na ni miongoni mwa wagombea watano wa tuzo ya mchezaji bora wa soka wa BBC Afrika mwaka huu.

Kwa upande wake meneja wa timu hiyo Jurgen Kloop amemwagia sifa mchezaji huyo 

"Siwezi kufikiria klabu yoyote Ulaya ambayo haiwezi kumtaka mchezaji kama Mane awachezee, kwahivyo kwamba anataka kuendelea kucheza na sisi, inatoa ujumbe kuhusu sehemu tuliopo kwa sasa," amesema meneja wa Liverpool, Klopp.

Mkataba wa Mane unafuata mikataba mingine kama hiyo ya muda mrefu kwa wachezaji wenzake Mane wa kiungo cha mbele, Roberto Firmino, aliyekubali mkataba huo mnamo Aprili, na Mo Salah, aliyesaini mkataba mpya Julai.

Chanzo:- Bbc 

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post