Friday, November 2, 2018

RAIS MAGUFULI : UONGOZI NI KAZI NGUMU SIKUTEGEMEA INGEKUWA NGUMU HIVI...

  Malunde       Friday, November 2, 2018
Rais John Magufuli amesema hakuna kipindi anachopitia changamoto katika uongozi kama ilivyo sasa.

Amesema kuongoza nchi ni kazi ngumu na wakati mwingine anashindwa kulala kutokana na kukabiliwa na mambo mengi ya kufanya.

Ametoa kauli hiyo jana mchana Alhamisi Novemba Mosi, 2018 katika kongamano la uchumi na siasa lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

“Uongozi ni kazi ngumu sikutegemea ingekuwa ngumu hivi. Yaani ukiingia chumbani kwangu mafaili yamejaa hadi kitandani na kila moja lina umuhimu huwezi kulipeka kwa mtu mwingine,” amesema.

Pia, amezungumzia jinsi anavyopenda kuzungumza lugha ya Kiswahili akibainisha kuwa ndio lugha inayowaunganisha Watanzania.

“Nasikia watu wanasema hajui Kiingereza nimekuwa waziri nikasafiri nchi nyingi kwenye vikao huko nilikuwa napewa uongozi wakati mwingine wa mikutano mikubwa sasa nilikuwa nazungumzaje kama sijui, “ amesema.

“Ukiniambia kusafiri sijui wapi sijafika, nimetembea karibu dunia yote kwa sasa sina haja kwangu ni Utanzania kwanza na kipaumbele changu ni kuwatumikia Watanzania.”
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post