DUDU BAYA 'OIL CHAFU,MAMBA' ATINGA POLISI SAKATA LA MASHOGA

Msanii wa Hip Hop Bongo, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’, ametinga katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam kuitikia wito wa jeshi hilo ikiwa ni siku chache baada ya kuanika hadharani majina ya watangazaji wa kiume wanaojihusisha na vitendo vya ushoga.

“Naelekea kituo cha Polisi kuitikia wito wa jeshi, nikipelekwa gerezani kwa ajili ya hawa mashoga naomba ndugu yangu yeyote asiniletee chakula, nitashinda na kulala njaa lakini nitapigana kuishinda hii vita ambayo hata vitabu vya dini vimeilaani.” Amesema Dudu Baya.

Dudu Baya ambaye anajiita Oil Chafu, Konki Konki Konki Master, Mamba amefika Ostabay Polisi kwaajili ya kuhojiwa na Mkuu wa Upelelezi kuhusiana na orodha yake aliyoitoa mtandaoni ya watu aliodai wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post