POLISI WAMSHIKILIA KAKA WA RAIS KWA TUHUMA YA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA


Kaka wa Rais wa nchi ya Honduras, Juan Orlando Hernandes amekamtwa na polisi kwa kosa la kufanya biashara ya madawa ya kulevya, silaha na kuweka taarifa za uongo, kwa mujibu wa idara ya mahakama ya Marekani.
Mamlaka zinazohusika na kudhibiti madawa ya kulevya zilimkamata Antonio Hernandes Alvara ambaye pia anajulikana kama 'Tony Hernandes', akiwa mjini Miami, lakini anashtakiwa New York nchini Marekani.

Hernandes mwenye miaka 40 ambaye pia ni mbunge, anahusika na kusafirisha tani nyingi za madawa ya kulevya aina ya cocaine yanayoingia Honduras kwa ndege, boti, na huwekwa lebo ya jina lake ya 'TH”.

Pia Hernandes husafirisha madawa hayo kwa ulinzi mkubwa wenye silaha za moto, ndani ya nchi ya Honduras, akiwa na baadhi ya askari polisi wa taifa hilo la Honduras.

Mwaka 2014 ilinaswa sauti yake akikutana na Davis Leonel Rivera ambaye ni kiongozi wa wafanyabiashara ya madawa ya kulevya wa Honduras, ambao wenyewe wanajiita 'Cachiros'.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527