BENKI YA ABC YAWEKEZA KWENYE MAENDELEO YA JAMII


Meneja wa Benki ya ABC tawi la Arusha Magabe Nyambuche akizungumza na waandishi wa habari
*** 
Benki ya ABC tawi la Arusha imeendelea na juhudi za kuwekeza kwenye maendeleo ya jamii kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali ,kusaidia jamii kupata bima za afya ili kuharakisha maendeleo ya jamii ya Kitanzania.

Meneja wa Benki hiyo tawi la Arusha Magabe Nyambuche amesema kwa mwaka 2019 Benki hiyo imejipanga kutoa mikopo kwa Vikundi maalumu ikiwemo Vicoba na Sacco's ambao wamekuwa wakipewa mafunzo na Maafisa wa Ustawi wa jamii ili waweze kunufaika na mikopo kwa kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Magabe alisema benki hiyo limekua karibu na jamii na kuwafikia wananchi walioko vijijini kupitia ubunifu wa kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ambapo benki hiyo ilipewa tuzo ya ubunifu.

"Kwa sasa tuna mawakala 250 ambao wanahakikisha kuwa wateja wetu wanafikiwa na huduma za kifedha popote pale walipo", alieleza Meneja hiyo.

Hata hivyo benki hiyo imedhamini mkutano mkuu wa wadau wa maendeleo ya jamii unaoendelea jijini Arusha ikiwa ni juhudi mojawapo ya kuisaidia jamii ambayo hunufaika na utaalamu wa Maafisa wa Maendeleo katika Vijiji na Mjini.

Pia wamejizatiti katika kuendelea kushirikiana na serikali kuharakisha maendeleo ya jamii kwa kutuma dhana ya uwezeshaji wa mikopo yenye masharti nafuu.

Na Ferdinand Shayo,Arusha
Meneja wa Benki ya ABC tawi la Arusha Magabe Nyambuche akizungumza na waandishi wa habari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527