MAANDALIZI YA UJENZI WA BARABARA YA NJIA SITA YA UBUNGO-CHALINZE


Muonekano wa barabara ya Morogoro eneo la Kimara mwisho Jijini Dar es salaam hivi leo ambapo tayari maandalizi ya ule mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Ubungo hadi Kibaha Mkoani Pwani yenye urefu wa kilometa 16 umeiva.

 Ujenzi wa barabara hiyo unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huu utasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa katika nchi jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.

 Pia inatarajiwa utasaidia kupambana na changamoto ya msongamano wa magari na kuziwezesha barabara zote za Jiji la Dar es Salaam kupitika katika majira yote ya mwaka. 
Picha na IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527