BancABC YAJA NA OFA KWA WATEJA WA AKAUNTI ZA AMANA

Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi BancABC Joyce Malai (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Barton Mwasamengo wakionyesha bango baada ya benki hiyo kutangaza kutoa ofa maalum kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana ambapo Watapata riba ya asilimia 14 papo na inaanza leo Novemba mosi mpaka Disemba 31 mwaka huu.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi BancABC Joyce Malai (kushoto) kutangaza hatua ya benki hiyo kutoa ofa maalum kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana ambapo Watapata riba ya asilimia 14 papo na inaanza leo Novemba mosi mpaka Disemba 31 mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Barton Mwasamengo.
 ****


· Wateja wanaoufungua akaunti za amana kupata riba hadi asilimia 14 papo hapo. 

BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, imepiga hatua nyingine kwenye soko baada ya kutangaza ofa kabambe kwa wateja wakati huu wa kuelekea msimu wa Krismasi na sikukuu za mwisho wa mwaka. 

Ofa hiyo ni maalum kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana ambapo Watapata riba ya hadi asilimia 14 papo hapo, Ofa hiyo imeanza leo na wateja wote watanza kufaidika nayo kuanzia leo Novemba mosi mpaka Disemba 31 mwaka huu. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza hatua ya benki hiyo kutoa ofa hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi BancABC Joyce Malai alisema kuwa benki yake imeamua kutoa ofa hadi asilimia 14 ya papo kwa papo kwa wateja wote ambao wanafungua akaunti za amana. 

Hata hivyo, Malai alisema wateja watakuwa na uhuru wa kuchangua kuchukua riba papo hapo au kwa kila mwezi au mwishoni mwa amana. Vile vile, mteja atakuwa na uwezo wa kuchukua mkopo wa hadi asilimia 80 ya amana yake, Malai aliongeza. Hii ni ofa bora kwenye soko kwa sasa na hivyo tutoa wito kwa wateja wetu na hata wale wasiokuwa na akaunti kwetu kutumia fursa ya ofa hii ya msimu huu wa sikukuu kwa manufaa yao,” alisema alisema Malai. 

Malai alisema kuwa BancABC imejidhatiti kufikia mahitaji ya wateja na kuhakikisha kwamba wanakua pamoja na benki hiyo. “Tunathamini jinsi wateja wetu wanavyotuunga mkono na hiyo ndio sababu sisi kama benki tumeamua kuwazawadia ofa hii kabambe katika msimu huu wa sikukuu,”. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Barton Mwasamengo “Kinachotakiwa kufanywa na mteja yeyote ili aweze kujipatia ofa hii nikufika kwenye matawi yetu nchini kote na kufungua akaunti ya amana ya muda maalumu ambapo riba hiyo italipwa papo hapo, lengo ni kukupa uhuru wa kuitumia kwa ajili ya kufanya manunuzi binafsi kama upendavyo ikiwemo kununua zawadi kwa familia au marafiki ili kuwaongezea furaha katika msimu huu wa sikukuu,” aliongeza Malai. 

Mwasamengo aliongeza kuwa ofa hiyo itawahusu wateja watakaofungua akaunti za amana za muda maalumu BancABC na ofa hii inaanza leo Novemba mosi mpaka Disemba 31 mwaka huu. “Tunataka msimu huu wa sikukuu kuwa mzuri zaidi kwa wateja wetu kwa kuwa tunafahamu kwamba watu wengi hutumia kiasi kikubwa cha fedha wakati wa Krismasi. Kupitia riba hii watakayopata awali, wataweza kupata mahitaji yao kirahisi,” alisema. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post