Thursday, October 11, 2018

WAZIRI NDUGULILE MGENI RASMI MKUTANO WA FURSA KWA WANAMUZIKI JIJINI DAR ES SALAAM

  Malunde       Thursday, October 11, 2018


NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile kesho kutwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa fursa kwa wanamuziki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga alisema mkutano huo ni muhimu sana kwao.

"Mkutano huu utakaofanyika kesho kutwa ni muhimu sana kwetu kwani utawakutanisha wanamuziki mbalimbali hivyo ni vema wanamuziki wakajitokeza", alisema Dk.Kisanga.

Dk.Kisanga alisema katika mkutano huo Ndugulile atapata fursa ya kugawa kadi za matibabu za mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) katika ukumbi wa NSSF Ilala.
Na Dotto Mwaibale - Dar es salaam
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post