Picha : UN,TEF WAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA KUHUSU MIRADI YA MASHIRIKA YA UN TANZANIA

Umoja wa Mataifa (UN) kwa kushirikiana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) umeendesha mafunzo kuhusu Miradi ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa Waandishi wa habari wa mikoa ya Kanda ya Ziwa (Mwanza,Mara,Shinyanga na Simiyu). 

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Jumatano Oktoba 17,2018 katika ukumbi wa Hoteli ya Adden Palace Jijini Mwanza. 

Akifungua mafunzo hayo,Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwa ajili ya kufuatilia miradi inayotekelezwa na Mashirika ya Umoja wa mataifa nchini Tanzania. 

Balile aliwataka waandishi wa habari kuandika habari za kuhamasisha wananchi ili kuleta maendeleo katika nchi.

Hata hivyo Balile alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waandishi wa habari kujiendeleza kielimu,kuandika habari za uchunguzi pamoja na kuandika habari za maendeleo badala ya kujikita katika habari za kukosoa pekee. 

Awali akizungumza,Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Neville Meena alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kufuatilia na kuujulisha umma kuhusu Miradi inayotekelezwa kwa ubia baina ya serikali ya Tanzania na Mashirika yaliyopo chini ya Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa pamoja uitwao UNDAP. 

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza,Simiyu,Mara na Shinyanga katika ukumbi wa Hoteli ya Adden Palace Jijini Mwanza leo Jumatano Oktoba 17,2018. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile akizungumza wakati wa mafunzo hayo na kuwasisitiza waandishi wa habari kujiendeleza kielimu,kujikita katika habari za uchunguzi na kuandika habari za maendeleo.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Neville Meena akielezea malengo ya mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu miradi inayotekelezwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Neville Meena 
Afisa Mawasiliano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Warren Bright akielezea kuhusu mashirika ya Umoja wa Mataifa na Miradi mbalimbali inayotekelezwa na mashirika 23 ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania.
Afisa Mawasiliano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Warren Bright akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo.
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Mkufunzi Allan Lawa akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.

 Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post